“Ole wake atakayefanya biashara nje ya masoko ya madini”- Biteko
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Wizara ya Madini, Doto Biteko akiwasilisha salamu za Wizara hiyo kwenye ziara ya Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida, hii leo Februari 20, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) ameungana na viongozi mbalimbali kushiriki katika ziara ya Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (hayuko pichani) mkoani Singida ambapo katika Wilaya ya Iramba, Mama Samia amekagua kiwanda cha kusindika mafuta ya alizeti cha Yaza kinachomilikiwa na mwekezaji mzawa kilichopo eneo la Ndago, ujenzi wa Kituo cha Afya Kinampanda pamoja na ukarabati wa Chuo cha Ualimu Kinampanda na baadae kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
Waziri wa
Madini, Doto Biteko amesema Serikali kupitia Wizara hiyo inatarajia kuanzisha
masoko ya madini hapa nchini, hivyo wafanyabiashara wote watapaswa kuuzia
madini yao kwenye masoko hayo.
Biteko
ametoa kauli hiyo hii leo kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais, Mama
Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Kinampanda, Wilaya
ya Iramba mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi aliyoianza
Februari 16, 2019 mkoani humo.
Tazama BMG Online TV hapa chini
SOMA>>> Makamu wa Rais akagua miradi ya maendeleo Mkalama mkoani Singida
SOMA>>> Makamu wa Rais akagua miradi ya maendeleo Mkalama mkoani Singida
No comments: