LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makamu wa Rais akagua miradi ya maendeleo Mkalama mkoani Singida

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan akikagua ujenzi wa daraja la Sibiti lililopo mpakani mwa wilaya ya Mkalama mkoani Singida na Meatu mkoani Singida, jana Februari 19, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kaimu Meneja wa TANROADS mkoani Singida, Mhandisi Matari Masige (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kuhusiana na ujenzi wa daraja la Sibiti.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Sibiti.
Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) akiwasilisha salamu za Wizara kwenye ziara hiyo.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi katika Kijiji cha Ibaga wilayani Mkalama.
Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso akisalimiana na binti Laila Ramadhan (19) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Iguguno wilayani Mkalama.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akimpongeza binti mwanafunzi Laila Ramadhan kwa juhudi zake katika masomo na kuwahimiza wazazi na waalimu wake wamlee vyema ili asome hadi elimu ya Chuo Kikuu.
Bwalo la JPM katika shule ya sekondari Iguguno wilayani Mkalama.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi mpya za Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida.
Mwonekano wa mbele wa ofisi za Halmashauri ya Mkalama zilizozinduliwa na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
Jengo la ukumbi katika ofisi za Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mkalama.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadharani wilayani Mkalama.
Tazam BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.