Mbunge Mabula atoa Milioni 22 ujenzi wa soko la Mlango Mmoja uanze haraka
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa
Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (CCM) ametoa shilingi
Milioni 22 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya soko la Mlango Mmoja iliyoteketea
kwa moto miezi mitatu iliyopita.
Mabula
aliyasema hayo jana baada ya kuwatembelea wafanyabiashara wadogo (machinga)
katika soko hilo na kubainisha kwamba fedha hizo kutoka mfuko wa jimbo zitasaidia
ujenzi wa paa lote.
Mwenyekiti
wa soko hilo, Jackson Kayoza alisema kulingana na tathmini iliyofanyika,
shilingi Milioni 98 zinahitaji kwa ajili ya ujenzi wa sehemu iliyoungua moto
hivyo alimshukru mbunge Mabula kwa mchango huo.
Mmoja wa
machinga katika Soko la Mlango Mmoja ambaye pia bidhaa zake zilitekeketea kwa
moto, Isaack Julius, alisema mchango wa mbunge Mabula uwe chachu kwa Halmashauri
ya Jiji la Mwanza kwa kuhakikisha inakamilisha kiasi cha fedha kinachohitajika
ili ujenzi huo uanze mara moja.
Septemba 28,
2018 majira ya alfajiri, ajali ya moto ilizuka katika Soko la Mlango Mmoja na
kusababisha meza 83 za wajasiriamali, maduka 23 na vyoo vitatu kuteketea ambapo
hasara yake haikujulikana mara moja.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (katikati), akizungumza na wafanyabiashara wadogo (machinga) katika Soko la Mlango Mmoja Jijini Mwanza.
Tazama BMG Online TV hapa chini