Benki ya Diamond Trust (DTB) yamuunga mkono Mbunge wa Nyamagana
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Benki ya
Diamond Trust (DTB) imekabidhi mifuko 100 ya saruji kwa mbunge wa jimbo la
Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM), ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za
maendeleo katika jimbo hilo.
Akizungumza jana
kwenye zoezi la kukabidhi mifuko hiyo, Ezra Shandu ambaye ni Meneja Msaidizi
DTB Tawi Kuu la Mwanza, alisema lengo ni kusaidia utatuzi wa changamoto
mbalimbali katika sekta ya elimu na afya ikiwemo ujenzi wa madara, vyoo pamoja
na wodi za afya.
Akipokea
mifuko hiyo ya saruji, mbunge Mabula aliishukru benki ya “DTB” na kubainisha
kwamba itasaidia kutatua changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo zaidi ya
elfu moja pamoja na vyumba vya madarasa takribani 900 katika jimbo la
Nyamagana.
Kutoka kushoto ni Meneja Msaidizi DTB Tawi Kuu la Mwanza, Ezra Shandu, Meneja DTB Tawi Kuu la Mwanza, Nabeel Alnoor, Mbunge jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula pamoja na Afisa Masoko DTB Tawi Kuu la Mwanza, Boniphace Mwita.
Tazama BMG Online TV hapa chini