LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ushindi wa kishindo uchaguzi Jumuiya ya Wazazi wilayani Nyamagana

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, wamemchagua kwa kura nyingi Peter John Bega (kulia) kuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo na kuwamwaga wagombea wenzake Joseph Kadege Bupamba (kushoto) pamoja na Mashaka Kamchape Kaguna (katikati) katika uchaguzi uliofanyika hii leo Januari 12, 2019 kwenye ukumbi wa "Hand Hall" Jijini Mwanza.

Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Charles Nyamasiriri kuchaguliwa kuwa diwani wa Kata ya Isamilo katika uchaguzi mdogo uliofanyika Aprili 2018 na hivyo kujiuzulu nafasi hiyo kama ambavyo kanuni za uchaguzi za CCM za mwaka 2017 zinavyoelekeza kwamba mwanachama mmoja anapaswa kuwa na cheo kimoja.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Dismas Masunu ambaye ni Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza akitangaza matokeo kwenye uchaguzi huo.
Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi CCM akiwemo Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama hicho wilayani Nyamagana (kushoto), wakiteta jambo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.