RC Mongella akagua ujenzi wa Hospitali ya Bwisya wilayani Ukerewe
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Ujenzi huo unaendelea vyema na unatarajiwa kukamilika kwa wakati mwezi ujao.
Hospitali ya Bwisya kisiwani Ukara inajengwa na kampuni ya SUMA JKT.
Na George
Binagi-GB Pazzo
Mkuu wa
Mkoa Mwanza, John Mongella jana Januari 16. 2019 amekagua upanuzi wa Kituo cha
Afya Bwisya kilichopo katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, kinachongengwa
kwa hadhi ya Hospitali ya Wilaya.
Itakumbukwa
kwamba Novemba 17, 2018 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo alizindua rasmi ujenzi wa miundombinu
katika Kituo hicho unaofanywa na kampuni ya SUMA JKT chini ya usimamizi wa Kamati
Maalum iliyoundwa na Mongella kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 800.
Huu ni
utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli aliyeagiza sehemu ya fedha za
rambirambi zilizopatikana kufuatia ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere kilichozama
Septemba 20, 2018 zitumike kufanya ukarabati katika Kituo cha Afya Bwisya ili
kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa kisiwa cha Ukara.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali mkoani Mwanza akikagua ujenzi wa Hospitali ya Bwsya wilayani Ukerewe.Ujenzi huo unaendelea vyema na unatarajiwa kukamilika kwa wakati mwezi ujao.
Hospitali ya Bwisya kisiwani Ukara inajengwa na kampuni ya SUMA JKT.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: