LIVE STREAM ADS

Header Ads

Sekou Toure yaibuka Hospitali Bora, Mongella ataka watumishi wapewe motisha

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (anayeongea) ameutaka uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwanza Sekou Toure, kuandaa utaratibu wa kutoa motisha kila mwezi kwa watumishi wa Hospitali hiyo wanaofanya kazi kwa juhudi zaidi.

Mongella alitoa rai hiyo jana kwenye kwenye hafla ya Benki ya CRDB kukabidhi hundi ya shilingi Milioni 20 katika Hospitali hiyo,  ili kusaidia ukarabati wa chumba cha upasuaji katika wodi ya akina mama hospitalini hapo.

Aidha aliwapongeza watumishi wa Hospitali ya Sekou Toure kwa juhudi zao zilizosaidia kuibuka Hospitali Bora nchini kwa mwaka wa pili mfululizo na hivyo kuwahimiza kuendelea na juhudi hizo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.