LIVE STREAM ADS

Header Ads

Haya ndiyo makadirio ya bajeti kwa mwaka 2019-20 Misungwi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazz0, BMG
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, leo Januari 18, 2019 limekutana kujadili makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2019/20.

Akiwasilisha makadirio hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Anna Urio amesema shilingi bilioni 56.5 zimekadiriwa kutumika kwa mwaka wa fedha 2019/20 ikiwa ni fedha za miradi ya maendeleo pamoja na matumizi mengineyo.

Makadirio hayo yameongezeka ikilinganishwa na makadirio ya mwaka uliopita ambapo Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi lilipitisha makadirio ya bajeti ya shilingi bilioni 51.7.

Akizungumza kwenye baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Antony Bahebe amesisitiza Serikali kuharakisha utoaji wa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo maji kwani kuna baadhi ya miradi inachelewa kukamilika kutokana na ucheleweshwaji wa fedha ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Kisena Mabuba ameahidi kuisimamia vyema hoja hiyo kwa kuiwasilisha Serikalini.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Misungwi, Antony Bahebe (kushoto), akizungumza kwenye baraza la madiwani wa halmashauri hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Kisena Mabuba.
Diwani wa Kata ya Buhingo, Marco Kadala akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Watendaji mbalimbali Halmashauri ya Misungwi akiwemo Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Anna Urio (kulia).
Watendaji mbalimbali Halmashauri ya Misungwi akiwemo Afisa Elimu Sekondari Mwl. Diana Kuboja (kushoto) pamoja na Afisa Elimu Msingi, Mwl. Frank Magabilo (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini
BARAZA LA MADIWANI: Maswali na Majibu papo kwa hapo

No comments:

Powered by Blogger.