RC Mongella- "Ongezeni kasi mradi ukamilike kwa wakati"
Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.
Na Georgr Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa
Mwanza, John Mongella ameeleza kutoridhishwa na kasi ya ukarabati wa Kituo cha
Afya Katunguru kilichopo katika Wilaya ya Sengerema na kuwaagiza viongozi
wilayani humo kusimamia ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati mapema mwaka ujao.
Mongella
alitoa kauli hiyo Disemba 18, 2018 baada ya kufanya ziara katika Kituo hicho
kilichopewa shilingi Milioni 400 na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa majengo
matano mapya ambayo ni nyumba ya mtumishi, maabara, wadi ya wazazi, jengo la
upasuaji pamoja na jengo la kuhifahia maiti kupitia mfumo wa “Force Account”. Tazama BMG Online TV hapa chini
Tazama habari zaidi hapo chini kutoka BMG Online TV
No comments: