LIVE STREAM ADS

Header Ads

MISUNGWI: Wahitimu wapewa dhamana ya kusukuma mbele maendeleo ya Taifa

Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.

Viongozi, waalimu na wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi (Misungwi CDTTI), wakiwa wameambatana na mgeni rasmi, Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Peter Sabatho (katikati) aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Sweda (hayuko pichani), wakiwasili katika viunga vya chuo hicho kuanza rasmi hafla ya Mahafali ya Nane ya Chuo hicho yaliyofanyika jana Disemba 07, 2018.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi mkoani Mwanza, wametakiwa kuyatumia vyema mafunzo na elimu waliyoipata kwa ajili ya maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi, Peter Sabatho alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Misungwi, Juma Sweda kwenye Mahafali ya Nane ya Chuo hiyo.

Makamu Mkuu wa chuo hicho kitengo cha Taaluma, Dongo Nzori Dongo alisema jumla ya wahitimu 193 wamehitimu chuo hapo katika ngazi za Cheti na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2017/18 na tayari kimedahili wanafunzi 230 kwa mwaka wa masomo 208/19.

Mkuu wa chuo hicho, Yahaya Msumi alisema kinatoa mafunzo katika ngazi za Cheti cha Msingi (Basic Technician Certificate), Cheti (Technician Certificate) na Stashahada (Ordinary Diploma) kwa kuratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu la Ufundi (NACTE) chini ya mfumo wa “NTA Levels”.

Msumi alisema chuo hicho kilianzishwa mwaka 1982 Mlale mkoani Ruvuma na mwaka 1983 kilihamishiwa Misungwi mkoani Mwanza na kuanza kutoa mafunzo ya Cheti cha Msingi cha Maendeleo ya Jamii Ufundi (Basic Certificate Course in Civil Engineering-BCC) na ilipofika mwaka 2008 kilibadilishwa Mitaala na kuanza Program za Uhandisi, Ujenzi na Maendeleo ya Jamii.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi, Yahaya Msumi akitoa utambulisho kwenye hafla hiyo.
Katibu Tawala Wilaya ya Misungwi, Peter Sabatho akizungumza kwenye Mahafali ya Nane ya Chuo cha Maendeleo Ufundi Misungwi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Sweda (hayuko pichani).
Makamu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii-Ufundi kitengo cha Taaluma, Dongo Nzori Dongo akizungumza kwenye mahafali ya nane ya chuo hicho.
Muadili (Dead of Students) wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii-Ufundi Misungwi akieleza historia fupi ya chuo hicho.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa Mwanza, Isaac Ndassa akiwasilisha salamu za Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Kisena Mabuba ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Ufundi Misungwi akiwasilisha salamu za Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo hicho.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi, Yahaya Msumi (kulia), akimkabidhi mgeni rasmi taarifa ya chuo hicho.
Baadhi ya wahitimu wakisalimiana na mgeni rasmi, waalimu wa chuo pamoja na viongozi mbalimbali.
Jumla ya wahitimu 193 wamehitimu chuo hapo katika ngazi za Cheti na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2017/18 na tayari kimedahili wanafunzi 230 kwa mwaka wa masomo 208/19.
Viongozi mbalimbali meza kuu.
Wahitimu
Brass band ikiongoza wahitimu na viongozi mbalimbali wakati wakiwasili eneo la tukio.
Wahitimu na watumishi wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii na Ufundi Misungwi wakiwasili eneo la mahafali.
Baadhi ya watumishi na wahitimu wakiingia eneo la tukio.
Wahitimu.
Baadhi ya wahitimu
Wahitimu.
Wahitimu.
Tazama BMG Online TV hapa chini

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo, BMG

No comments:

Powered by Blogger.