Wachimbaji madini Mahenge mkoani Morogoro watakiwa kulipa madeni yao
Wasiliana na BMG Blog/ BMG Online TV kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma ya Habari na Matangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Serikali
kupitia Wizara ya Madini imeondoa zuio la kuyafunga machimbo ya madini ya vito ya Epanko yaliyopo Mahenge Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro huku ikiwataka
wamiliki wote wa leseni katika machimbo hayo kulipa madeni yao.
Naibu Waziri
wa Madini, Doto Biteko ameyasema hayo leo Disemba 14, 2018 wakati akizungumza
na wachimbaji madini wilayani Ulanga na kueleza kwamba wapo baadhi ya
wachimbaji wanadaiwa na serikali hadi shilingi Milioni 200 hivyo wahakikishe
wanalipa madeni hayo kuanzia jumatatu vinginevyo Serikali haitasita
kuwanyang’anya leseni zao.
Amesema
Julai 10, 2018 Serikali iliyafunga machimbo ya Epango kutokana na baadhi ya
wachimbaji kutokuwa waaminifu na kukiuka sheria na taratibu za uchimbaji
ikiwemo ukwepaji kodi na maduhuli mbalimbali ya Serikali.
“Kila
mchimbaji tulimuuliza umewekeza nini, umeajiri wafanyakazi wangapi, umepata
faida kiasi gani, unauza wapi madini na umelipa kiasi gani Serikalini na
tukagundua udanganyifu mkubwa ambapo kuna wengine walikuwa na mauzo hadi
Milioni 900 lakini wameilipa Serikali Milioni nne tu”. Amesema Biteko.
Mkuu wa
Wilaya Ulanga, Ngollo Malenga ameahidi kusimamia maelekezo yote ili kuhakikisha
uwepo wa madini katika wilaya hiyo unachochea maendeleo katika jamii na Taifa
kwa ujumla.
Nao baadhi
ya wachimbaji waliohudhuria kikao hicho wameishukru Serikali kwa kuwapa ridhaa
ya kuendelea na shughuli zao na kuomba iwasaidie kutatua migogoro ya baina yao na wananchi ambayo
imekuwa ikiwakwamisha.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji madini Mahenge wilayani Ulanga.
Mkuu wa Wilaya Ulanga, Ngollo Malenga akitoa salamu zake kwenye kikao hicho.
Kamishna Tume ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeka akiweka kumbukumbu sawa kwenye kikao hicho.
Afisa Migodi Mkazi Wilaya ya Ulanga akitambulishwa kwenye kikao hicho.
Baadhi ya wachimbaji wakifuatilia kikao hicho.
Viongozi na wachimbaji wakifuatilia kikao hicho.
Baadhi ya viongozi na wachimbaji madini wakifuatilia kikao hicho.
Baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Madini pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Ulanga wakifuatilia kikao baina ya Naibu Waziri Madini, Doto Biteko na wachimaji madini wilayani Ulanga.
Pamoja na kikao hiki, Biteko pia amefanya uzinduzi wa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wilayani Ulanga ili kushughulikia masuala ya wachimbaji madini.
Tazama BMG Online TV hapo chini wakati machimbo ya Epanko yanafungwa, Julai 10, 2018