LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ukosefu wa vyoo wahatarisha afya za wavuvi wilayani Ilemela

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Afisa Mfawidhi wa Ulinzi wa Raslimali za Uvuvi Kanda Kuu ya Ziwa Victoria, Didas Mtambalike akizungumza na wananchi pamoja na wavuvi wa mwalo wa Bwiru  Kijiweni wilayani Ilemela.

Judith  Ferdinand, Mwanza
Afisa Mfawidhi wa Ulinzi wa Raslimali za Uvuvi Kanda Kuu ya Ziwa, Victoria Didas Mtambalike ameunda kamati maalum ambayo itasimami ujenzi wa choo katika Mwalo wa Bwiru  Kijiweni uliopo wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

Hii ni kutokana na  wakazi wa mwalo huo  kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa choo kwa muda mrefu na hivyo kulazimika kujisaidia katika maeneo  ambayo siyo rasmi na kuhatarisha afya zao.

Mtambalike alilazimika kuunda kamati hiyo baada ya wananchi wa maeneo hayo  kulalamikia ukosefu wa choo kwa muda mrefu wakati akizungumza nao kwenye mkutano uliofanyika mwaloni hapo sanjari na kutumia fursa hiyo kuagiza kamati hiyo kufanya utafiti wa eneo lipi ambalo linafaa kwa ujenzi nje ya mita sitini kutoka ziwani.

Pia Mtambalike alitumia fursa hiyo kuwahimiza wananchi wa maeneo hayo kuanzisha ushirika wa wavuvi  katika mwalo huo ili uweze kuwasaidia katika masuala mbalimbali ikiwemo kujiinua kiuchumi.

Naye  Afisa Uvuvi wa Halmashauri ya Manispaa  ya Ilemela, Musa Mukonga alisema halmashauri hiyo inaendelea kuimarisha miundombinu  katika mialo yote ambapo imetenga shilingi milioni 300 kwa ajili ya kufanya maendeleo kwenye sekta ya uvuvi.

No comments:

Powered by Blogger.