Zahanati ya John Mongella yarahisisha huduma za afya kwa wananchi
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
SOMA>>> Jumuiya ya ALAT Mwanza yaeleza ilichobaini halmashauri ya Misungwi
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Wajumbe wa
Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT) tawi la Mkoa wa Mwanza wametembelea
zahanati ya John Mongella iliyopo katika Kijiji cha Bundilya wilaya Magu mkoani
Mwanza na kuridhishwa na ujenzi wa zahanati hiyo.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya wilaya Magu, Lutengano Mwalwiba amesema ujenzi wa zahanati
hiyo umegharimu shilingi milioni 54 ikiwa ni fedha za halmashauri, wananchi
pamoja na wahisani.
Mmoja wa
akina mama aliyefika katika zahanati hiyo kupata huduma amesema imewaondolea
usumbufu wa kufuata huduma za afya umbali mrefu na hivyo kuomba serikali
iendelee kuboresha huduma ikiwemo kuongeza watumishi wa afya pamoja na dawa.
Mwenyekiti
wa ALAT mkoani Mwanza, Hilali Elisha ambaye pia ni Mwenyekiti halmashauri ya
Magu amesema jambo kubwa la kujifunza katika halmashauri hiyo ni matumizi
sahihi ya fedha kupitia utaratibu wa “Force Account” ambapo miradi mingi ya
maendeleo ikiwemo afya, elimu na maji imetekelezwa vyema kwa gharama nafuu.
SOMA>>> Jumuiya ya ALAT Mwanza yaeleza ilichobaini halmashauri ya Misungwi
No comments: