Wafanyakazi ATCL watakiwa kutanguliza uzalendo
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Watendaji na
wafanyakazi wa shirika la ndege nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kwa
uadilifu ili kutanua wigo wa utoaji huduma.
Mkuu wa
wilaya Magu Mhe. Philemon Sengati ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa
Mwanza Mhe. John Mongella kwenye jukwaa la biashara la ATCL lililofanyika
Jijini Mwanza.
"Wafanyakazi
wote kwa maana ya bodi, menejimenti mjitoe kwa moyo na kuchapa kazi kwa
uzalendo, uaminifu, uhadilifu na kutoa huduma bora ili kampuni hii ipanuke na kuleta
faida kwa taifa. Alisema Sengati.
Mkurugenzi
Mkuu wa ATCL Mhandisi , Ladislaus Matindi
alisema serikali imeboresha huduma
na kulifufua shirika hilo, ili
kulifanya lifanye kazi kwa ufanisi, hivyo katika kuhakikisha wanazingatia hayo
hawatoruhusu kutengeneza madeni ya serikali kwa viongozi wake kutumia huduma ya
ndege hizo bila kulipa.
"Ili
kuhakikisha shirika letu linafanya kazi kwa ufanisi na kuacha kutengeneza
madeni ya serikali, kila kiongozi wake anayetumia usafiri wa ndege zetu lazima
halipe na kwa hili sitakuwa na mzaha lazima tuwe na nidhamu mfano hivi
karibuni Rais Magufuli alitumia ndege hizo katika safari zake alilipa
na amezingatia utaratibu sasa kama mwenye mamlaka amethubutu je
watendaji wake kwanini wasilipe,"alisema Mhandisi Matindi.
Hata hivyo
Meneja Mauzo na Usambazaji wa ATCL Edward Nkwabi alisema, kutokana na idadi ya
ndege walizonazo kwa sasa, wameanzisha safari ya kwenda Entebe (Uganda) na Bujumbura (Burundi)
ambayo ilianza Agosti 2018 baada ya kupokea ndege mbili aina ya A220-300, wamepanga
kuongeza safari ndani na nje ya nchi ikiwemo
Mpanda, Kahama, Iringa pamoja na
Mumbai nchini India), malengo ya mbele
wakipata ndege nyingine watapanua wigo hadi nchi za Afrika Magharibi, Ulaya na
Amerika Kaskazini.
Mmoja wa
washiriki wa jukwaa hilo, Eric Hamissi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Kampuni ya
Huduma za Meli (MSCL) alisema shirika hilo linaleta mapinduzimakubwa katika
usafiri wa anga hivyo alitumia fursa hiyo kuliomba kuanzisha safari za Mwanza
hadi Dodoma ambako ndio makao makuu ya nchi yalipo kwani kwa sasa wanapata
tabu wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa
kwani hadi wapitie Dar es salaam na gharama
inaongezeka.
No comments: