Mkuu wa Mkoa Mwanza akabidhi pikipiki kwa Maafisa Elimu
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa
Mwanza Mhe. John Mongella amekabidhi pikipiki 18 kwa Maafisa Elimu Kata katika
Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana), lengo likiwa ni kuchochea ufanisi na
utendaji kazi ndani ya Kata zao.
Akizungumza
kwenye hafla fupi ya kukabidhi pikipiki hizo iliyofanyika leo Septemba 10, 2018
katika ofisi za Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mhe. Mongella amewataka Maafisa
Elimu hao kuzitunza na kuzitumia vyema kwa matumizi yaliyokusudiwa.
Pikipiki
hizo zimetolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wa elimu kupitia program ya EQUIP-T na LANES zikiwa na thamani ya shilingi
Milioni 54.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo
Maafisa Elimu Kata na waalimu Jijini Mwanza wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella
Tazama BMG Online Tv hapa chini
No comments: