LIVE STREAM ADS

Header Ads

BUNDA: Biteko atoa maamuzi sakata la mwekezaji kuwatimua wanakijiji

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameitaka kampuni ya Lake Victoria Resources inayomiliki leseni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu katika Kijiji cha Kunanga wilayani Bunda, kuhakikisha inawalipa fidia wananchi wa kijiji hicho kabla ya kuanza shughuli zake za uchimbaji.

Biteko ametoa agizo hilo leo Septemba 21, 2018 alipokutana na wanachi wa Kijiji hicho, wachimbaji wadogo wa dhahabu pamoja na Mkurugenzi wa kamouni hiyo Ahmed Magoma,, baada ya kuwepo malalamiko kwamba wananchi hao wametakiwa kupisha maeneo yao ndani ya siku saba huku wakiwa hawajalipwa fidia.

Hatua hiyo ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli ambaye Septemba 05, 2018 akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoani Mara, alipokea malalamiko kutoka kwa wanakijiji hao wakimlalamikia Mkurugenzi wa kampuni hiyo kuwatimua kwenye maeneo yao bila fidia.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza kwenye mkutano huo
Wakazi wa Kijiji cha Kunanga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko
Tazama BMG TV Online hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.