LIVE STREAM ADS

Header Ads

Biteko achangia ujenzi wa shule mbili Bukombe, ajibu kero ya umeme

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mbunge wa jimbo la Bukombe mkoani Geita, Doto Mashaka Biteko (CCM) amekabidhi shilingi laki tano kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Msasa iliyopo jimboni humo.

Biteko ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini, alikabidhi fedha hizo papo hapo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika Kijiji cha Msasa, kufuatia ombili lililotolewa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Adam Mkwaba.

Pia Biteko alitoa ahadi ya mabati 80 kwa ajili ya uezekaji katika shule ya msingi Msambi ambapo alitumia mkutano huo kuwapongeza wananchi kwa kushiriki ipasavyo kwenye miradi ya maendeleo na kwamba serikali itaendelea kuwaunga mkono.

Pia aliwatoa hofu wakazi wa jimbo la Bukombe kuhusu upatikanaji wa huduma ya umeme ambapo alibainisha kwamba huduma hiyo itafika kila Kijiji kupitia mradi wa REA awamu ya tatu ambao utekelezaji wake umeanza jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Mashaka Biteko (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini akizungumza jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Masasa Kata ya Runzewe Magharibi jimboni humo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Masasa Kata ya Runzewe Magharibi, Adam Mkwaba akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Runzewe Magharibi wilayani Bukombe, John Nguhi akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Namonge wilayani Bukombe, Mlalu Bundala akizungumza kwenye mkutano huo.
Tazama hapa chini BMG Online Tv

SOMA>>>Biteko apata mapokezi makubwa jimboni, achangia miradi ya maendeleo

No comments:

Powered by Blogger.