Baraza la Wazee wilayani Ilemela lafanya uchaguzi
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, BMG
Baraza la
Wazee wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza limehimizwa kutumia chombo hicho
kujadili masuala ya wazee pamoja na kuishauri serikali katika nyanja mbalimbali
yakiwemo ya kimaendeleo.
Mkurugenzi
wa Halmashauri hiyo, Paul Wanga aliyasema hayo jana kwenye uchaguzi wa
viongozi mbalimbali wa baraza hilo na
kuongeza kwamba chombo hicho sio cha kisiasa bali kimewekwa kwa ajili ya
kuwakutanisha wazee ili kuzungumza mambo
yanayo wahusu sanjari na kuishauri Serikali ili kufikia uchumi wa viwanda.
"Baraza
limeanzishwa na Serikali kwa lengo mahususi la kuwakutanisha wazee pamoja na kujadili masuala yanayowahusu
sanjari na kuishauri, msitumike kisiasa
kwani siyo la itikadi ya chama chochote, badala yake tumieni ushawishi mlionao kuleta maendeleo ya wilaya
na taifa kwa ujumla". A alisema Wanga.
Alitumia
fursa hiyo kuliomba baraza hilo kuandaa katiba ambayo ndio itakuwa muongozo na
nyenzo muhimu yenye malengo mahususi ya kusaidia na kuwasilisha masuala mbalimbali
ya wazee.
Naye Mwenyekiti
wa baraza hilo, Mohamed Yusuph alisema itikadi ya nchi ni kuonyesha uzalendo na
kuwa wamoja hivyo viongozi ngazi ya Wilaya na Kata wanatakiwa kutumikia wazee
na kupaza sauti kwa serikali.
Baraza hilo
lilifanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali ikiwemo ya Mwenyekiti ambapo nafasi
hiyo alishinda Mohamed Yusuph aliyepata
kura 17, akifuatiwa na Malingumu Sospeter aliyepata kura 14, Kelege Venance kura
saba, Michael Urio akipata tano huku kura moja ikiharibika ambapo jumla ya kura
zilizopigwa ni zilikuwa 44.
Makamu
Mwenyekiti alichaguliwa Prisca Mwisijo baada ya kupata kura 28 kati ya 44
zilizopigwa dhidi ya Janeth Mussa aliyepata 16, huku Katibu akiwa Ndibayukao
Muchunguzi aliyepata kura 19 na Katibu Msaidizi akiwa Jackson Kabote aliyepata
kura 12.
Nafasi
nyingine ni Mweka Hazina ambapo Daniel Makolele aliibuka na ushindi wa kura 35
kati ya 44 zilizopigwa dhidi ya Hamisi Yona aliyepata tisa, huku Saulo Msumari
na Mary Selemani wakishinda nafasi ya uwakilishi wa baraza.
No comments: