LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bodaboda mkoani Mwanza wapewa semina na EWURA CCC

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Mhe. Dkt. Philis Nyingi amewapongeza bodaboda kwa juhudi zao za kuimaisha ulinzi na amani na kuwahimiza kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali pindi waonapo viashiria vya uvunjifu wa amani katika maeneo yao.

Ameyasema hayo wakati akifungua semina kwa viongozi wa bodaboda mkoani Mwanza iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) Mkoa Mwanza, iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Aidha Mhe. Dkt. Nyimbi ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa Mwanza amewahimiza bodaboda na watumiaji wengine wa huduma za nishati na maji kutoa taarifa pindi waonapo mtoa huduma anakiuka kanuni na sheria zinazomlinda mteja huku nao wakitimiza wajibu wao ikiwemo kulipia kwa wakati ankra na malipo mbalimbali ili kupata huduma endelevu.

Katibu Mtendaji EWURA CCC Taifa, Mhandisi Goodluck Mmari amesema lengo la semina hiyo ni kutoa elimu kwa watumiaji wa huduma za nishati na maji kwa kundi la bodaboda ili aweze kutambua haki na wajibu wao hatua itakayosaidia upatikanaji wa huduma bora kuelekea kwenye uchumi wa kati.

Naye mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Makoye Kayanda ambaye ni dereva bodaboda Jijini Mwanza amelishukuru Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji na kuongeza kwamba elimu waliyoipata itawasaidia kuongeza uwajibikaji baina ya watoa huduma na wateja.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana Mhe. Dkt. Philis Nyimbi akifungua semina hiyo
Katibu Mtendaji EWURA CCC Taifa, Goodluck Mmari akizungumza kwenye semina hiyo
Mwenyekiti wa Kamati la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji Mkoa Mwanza (RCC), Peter Niboye akizungumza kwenye semina hiyo
Picha ya pamoja

No comments:

Powered by Blogger.