LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA ELIMU KWA WADAU KUHUSU UALIBINO JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ufunguzi wa semina kwa wadau wanaosaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watu wenye ualibino, inayofanyika kwa siku nne kuanzia leo Jijini Mwanza. 

Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun ambapo imelenga kupanua uelewa kwa wanajamii/ wadau  kuhusu ualibino ili kusaidia kupambana na ukatili kwa watu wenye hali hiyo.
Binagi Media Group
Mwasisi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun, lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, akizungumza na wanahabari kwenye semina hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye mahojiano na Mwasisi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun, lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash.
Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun nchini Tanzania, Bi.Vicky Ntetema, akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun nchini Tanzania, Bi.Vicky Ntetema, wakati wa semina hiyo.
Mkufunzi Dr.George Rhoades kutoka nchini Marekani, akitoa elimu kuhusu ualibino kwenye semina hiyo.
Mkufunzi Dr.George Rhoades kutoka nchini Marekani, akitoa elimu kuhusu ualibino kwenye semina hiyo.
Kulia ni Mwasisi wa shirika la UTSS Peter Ash na kushoto ni Mkurugenzi wa UTSS nchini Tanzania, Vicky Ntetema
Mmoja wa washiriki wa semina akichangia mada
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo, akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ualibino mkoani Mwanza, Alfred Kapole (katikati).
 Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino duniani, Under The Same Sun, limebainisha kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualibino nchini vinaendelea kupungua.

Mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Vicky Ntetema, ameyasema hayo leo Jijini Mwanza kwenye semna kwa wadau wanaofanya kazi kwa ukaribu na watu wenye uaribino kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo za kijamii, elimu na afya.

Ntetema amesema elimu inayoendelea kutolewa kwa wanajamii imesaidia kupunguza ukatili kwa watu wenye ualibino ikiwemo kukatwa viungo na mauaji licha ya kwamba kumekuwepo taarifa za makaburi ya watu wenye ualibino waliofariki kufukuliwa katika mikoa ya Kagera, Mbeya na Morogoro.

Mwasisi wa shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya wanafunzi zaidi ya 300 wenye ualibino wanaosomeshwa na shirika hilo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo amewasihi wanajamii kuondokana imani potofu juu ya watu wenye ualibino ili kutokomeza ukatili dhidi yao.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, amesema serikali imelenga kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualibino vinatokomezwa ambapo amesisitiza elimu zaidi kuendelea kutolewa kwa wananchi ili kufanikisha lengo hilo.

No comments:

Powered by Blogger.